TUHOJIANE
BLOGU HII INATOA MADA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MAMBO YANAYOTOKEA KATIKA JAMII ZETU. UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI AMBAYO YATASAIDIA KATIKA KUELIMISHA WASOMAJI WENGINE. MAWAZO YANAYOTOLEWA HUMU SIO MSIMAMO WA MMIRIKI WA BLOGU HII.
Sunday, December 9, 2018
STUDENTS' CLUBS IN SCHOOLS
We all know the responsibilities of students in schools. Despite all what they study in classroom environment still they have also been engaging themselves in different extra works during their free time. Some of students like mostly to participate in sports and games. Playing in schools is the most common thing to students than doing things like gardening, planting of trees and other productive works.
My sincere thanks today are directed to 'FEMA' a noble Club, which has shown an excelling outstanding results to many schools. FEMA club in schools helps students to be aware of many things including self awareness and accountability to whatever they face in their lives. My advice to FEMA Coordinators is that they should keep on emphasizing students to keep in touch with their sensitive education through magazines and other posters. Educative seminars and workshops should also be part of the FEMA duties for helping students who by their ages they are vulnerable to different challenges in their daily life.
Teachers have also been part of this club and they are playing big role to students counselling and guidance. They should not loose hope rather they should keep on helping students. We appreciate you Teachers, well done! congratulations to FEMA for bringing this idea of establishing a sensitive club for our young generation.
BIG UP Nkoasenga secondary school,
Teachers and Students,
FEMA Club.
Students and their Teacher, Learning session,
FEMA CLUB, Nkoasenga secondary school
Good moments after club session.
Here we see students at Nkoasenga secondary school and their Teachers learning during FEMA Club.
FEMA Leaders if possible I ask you to make school visit to some schools which are not members of FEMA club.
USHIRIKI WA KAZI ZA ZIADA KWA WANAFUNZI
Kazi kubwa kwa Mwanafunzi shuleni ni kujifunza kulingana na mihutasari iliyowekwa na Wizara ya Elimu. Pamoja na hili jukumu muhimu pia Mwanafunzi anatakiwa ajihusishe na kazi za ziada kama kufanya usafi katika mazingira ya shule, kushiriki kazi za elimu ya kujitegemea na kujiunga na clubs mbalimbali kama FEMA, MALI HAI, SUBJECTS CLUBS, PCCB CLUB, SCOUT na zinginezo nyingi.
Mwanafunzi anapojihusisha na hizo kazi za ziada nje ya darasa zinamjenga katika kujitambua zaidi na kuwa raia mwenye kuwajibika katika maisha yake. Hali hiyo humpa muda wa kushirikiana na wenzake na kuwa na mtazamo chanya katika kazi za kizalendo za kujenga Taifa.
Kwa hisani ya Nkoasenga Sekondari, ARUSHA
Saturday, July 9, 2016
YAJUE MAHUSIANO.
KWA WANAWAKE NA WANAUME WOTE WANAOTARAJIA KUINGIA AU WALIOPO KWENYE NDOA.
Nafahamu mlio wengi hampendi kusoma vitabu vinavyotoa Elimu ya mahusiano,mkienda shopping mnaishia kununua nguo,urembo,na chakula cha familia tu wala hamuoni kuwa kuna umhimu wa kupita bookshop upate japo nakala 1 ya kitabu kitakachokupa ujuzi wa kumlea huyo Mke au Mme wako.!! Ikumbukwe kuwa sio vitabu vyote vyaweza kukupa maarifa mazuri bali uchuje kabla ya kutekeleza. Kama lugha ya vitabu vingine itakuwa ngumu ( kingereza ) waweza pia kupata elimu hii kwa njia zingine ndani ya jamii kwa watu wanaojiheshimu na kujali maadili yetu ya kiafrika na misingi ya imani za dini yako.
.
.
Haijalishi ni msomi wa kiwango gani bado kumbuka Elimu ya mahusiano haifundishwi sekondari wala chuokikuu. Hata hao wataalam wa kufunda unyago yawezekana hawajakupa vitu vyote unavyotakiwa kuvitekeleza katika ndoa yako..
.
Usiishie tu kujifariji eti unajua,wakati moyo wako unakushuhudia kuwa ndoa yako iko na matatizo. Umekuwa mtu wa kuzunguka kuhudhuria maombezi kwa watumishi wa Mungu bila mafanikio,lazima ujue kuna wajibu wako unatakiwa ufanye kwa vitendo naye Mungu atabariki mahusiano yenu,usiishie kusema namwachia Mungu, hapana..
.
*TAFAKALI MAMBO HAYA YATAKUSAIDIA.*
.
.
Ni jukumu lako kuwa romantic kwa mumeo/mkeo. Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi yako kwa mume/mke wako.
Mtumie meseji mume/mke wako anapokuwa kazini, muda mwingine hata kama yupo nyumbani mnaangalia TV chati nae katika mitandao ya kijamii (whatsapp, Imo, Facebook etc) hata kama yupo mbele yako jifanye hujui halafu tuma msg nzuri.
Hii huleta faraja na ni njia mojawapo ya kuwa romantic kwa mwanaume au mwanamke wako. Jadiliana nae jinsi gani anavyokuvutia. Mnunulie zawadi hata leso, underware, perfume, viatu etc. Mnapokua mezani mkila pamoja labda nyama, mpe nyama kubwa kuliko zote.
Tumieni sauti zenu laini kubembelezana na kudekezana, muimbie wimbo mzuri na kutaniana mnapokua pamoja chumbani, acheni u-serious kama mpo kwenye kikao cha bodi ya Korosho,unajifanya kilawakati umekunja sura utazani upo kwenye mkesha wa maombi, loooo !! Aibu.
Mume au mke wako anaporudi toka kazini usimkaribishe huku umenuna utafikiri shabiki wa Arsenal aliekosa kombe baada ya msimu wa ligi kuisha.
Epuka kuwa mchafu, weka mwili wako msafi pale inapolazimu kama hauko na kazi zinazosababisha uchafu. Jiweke vizuri muonekano na mavazi yako, jua nini uvae na wakati gani.Haijalishi hali ya kiuchumi uliyonayo bali jiweke vizuri kulingana na kile kidogo ulichonacho, usilazimishe maisha ya gharama wakati huna uwezo huo.
Mkaribishe mwenza wako kwa kumkumbatia au kwa hali itakayompa amani na furaha, na asubuhi anapoenda kazini Muombee Mungu amwepushe na mabalaa na muombee mafanikio(sio lazima uombe kwa taratibu za kawaida bali mtamkie neno la baraka tu inatosha). Msupport, mshauri, muondoe uchungu, mfariji pale panapokua na matatizo, sio kazi ndogo kuwa mwanaume/mwanamke. Sasa ujinga uliopo kwa baadhi ya wanawake ni kujifanya wako bize na kuwaachia house girls kupokea waume zao watokapo kazini, hivi msichana wa kazi akimpokea mmeo kila siku na labda kinatabia ya kuvaa vibaya nguo unatarajia nini kwa mmeo? Umekaa kujipa matumaini eti Mme wangu mshika dini nani alikudanganya mwili wa mmeo nao umeshika dini !!? Acha uzembe mwanamke.
Nanyi wanaume wenye kukaa nje na familia kwa muda mrefu nusu mwaka au mwaka na zaidi eti uko bize kikazi huendi nyumbani kuonana na mkeo, unatengeneza mazingira gani hapo? mbaya zaidi hauko nje ya nchi,unashindwaje kusafiru japo mara chache siku kadhaa unaiona familia unarudi kazini kwako. Mfano mme uko Mtwara na mke yuko Mwanza, kama unajua thamani ya mapenzi yenu lazima tu utakuwa na utaratibu mzuri wa kuchokoka kwenda kumwona mwenzako au mnapanga kukutania mji mwingine kama Dodoma kwa mfano wangu hapo juu ili kurahisisha muonane hata weekend moja kila mwezi inasaidia.Usitengeneze mazingira ya kumuweka mwenza wako katika majaribu ya mahusiano nje ya ndoa, hatusemi kuwa naye karibu ndo dawa ya kutosaliti bali kuna wengine wanasababisha kusalitiwa pia.
Pale unapoona anapoteza matumaini ni kazi yako kumpa moyo ni wakati ambao anakuhitaji sana uwe karibu yake na sio kumkwaza tena. Usimfananishe na wanaume au wanawake wengine. Mwanamke mpikie mmeo chakula akipendacho, mfulie nguo zake, mvalishe nguo na mpeti peti akiwa anaumwa.
Muamshane asubuhi na mapema, na msilalamikiane kama mmoja wenu anatabia ya kukoroma. Acha Kiss iwe njia yenu ya kuwasiliana wakati mwingine. Soma vitabu kuelewa namna ya kuishi na mume au mke, usijifunze kutoka katika movie. Ya kwenye Muvi Mengi sio ya kweli. Muite mume au mke wako jina lake la utani pia muite jina lake halisi hata kama ni mkubwa sana kuliko wewe as far as he is comfortable with it.
Kumbuka Mwenyezi Mungu ameagiza wanawake kuwatii wanaume zao, na wanaume kuwapenda wake zao. Ndoa sio show off bali ni kujitoa kwa moyo wote. Hakuna jambo zuri kwa watu wawili wanaopendana kweli zaidi ya Ndoa na ukiona Mwanaume au mwanamke anasua sua kila ukimueleza suala la Ndoa, ujue huyo hayuko serious na huenda hajakuweka moyoni kuwa naye maisha yenu yote, fungua macho fanya maamuzi kabla hujapotezewa muda wako bila mafanikio ya kuishi naye pamoja. Usilazimishe mapenzi ya kuoa au kuolewa na mtu ambaye hakutaki, soma alama za nyakati na ufanye maamizi sahihi.
*msichana ama mwanamke jiepushe na Mambo ya kuweka kinyongo na kulipiza visasi,hasira,kunyimana unyumba,dharau,kujifanya hujui wajibu wake kama mke,kazi zote nyumbani umemwachia house girl,kununa kusiko na maana,kutosikiliza mme wake anataka nini na hupenda nini,unajijali mwenyewe na kadhalika* kinyume na hapo usimlaumu mmeo kukabwa na mchepuko. Michepuko inajua mazaifu ya mke aliyeolewa na ndio maana inaweza kumteka mme wa mtu kiurahisi. Kwa wanaume nao pia wajifunze kujua hisia za mke aliyenaye,kuwa karibu na kutochukulia kiurahisi kila analosema mke, mara nyingi wanawake hawako wazi kwa kila kitu bali hutumia lugha za vitendo na hisia katika kuwasilisha mambo yao, hapa kuna shida na ndoa nyingi zimekwama katika suala la kuijua saikolojia ya mwanamke. Ulimwengu wa kifikra alionao kichwani mwanaume sio lazima ufanane na ulimwengu wa kifikra alionao mwanamke kichwani. Mwanamke anahuruka ya kutaka kutambuliwa kuwa ni MALIKIA PEKEYAKE duniani kote na hakuna malikia mwingine zaidi yake katika wanawake wote duniani na kusikojulikana, hupenda atambuliwe yeye ni malikia anayeweza kila kitu kuanzia jikoni, sebuleni hadi kitandani. Haijalishi uzembe alionao bado atahitaji haki ya kuinuliwa juu kuliko mawingu, wanaume wengi hawako tayari kuona uzembe au madhaifu ya mke halafu wakae kimya bila kukemea na kukalipia,ifahamike kuwa hata MUNGU alisema hawa ni viumbe dhaifu.
Na mwanaume au mwanamke ukipata anayejua kukujali,kulea,kukupa raha uitakayo katika maisha yako kwa nini uhangaike na michepuko iliyojaa laana ambayo ni mawakala wa shetani ktk kuvunja taasisi imara ya ndoa iliyoundwa na Mungu mwenyewe?
Samahani kwa mwanaume au mwanamke ambaye hujaingia katika maisha ya ndoa, naamini ujumbe huu utakuwa na faida kwako pia baadae Mungu atakapokupa hitaji la moyo wako.
Wanaume nao wanawajibu mkubwa kabisa na wanaitwa KICHWA CHA FAMILIA. Lakini wengi wamekuwa sio kichwa kwa mujibu wa kutekeleza majukumu yao katika familia zao, Kila mmoja ajue nafasi yake katika mahusiano na atekeleze bila uzembe maana MAHUSIANO YA NDOA NI TAASISI PANA SANA na haina mtaalamu aliyehitimu na kurizika bali kila mmoja anaishi kwa kumsikiliza mwenzake.
Ni taasisi ya Ndoa pekee ambapo wahusika hutunukiwa Vyeti kabla hata hawajaanza kusoma kozi za Chuo kikuu cha Mahusiano. Vyeti hutolewa mapema huenda jamii ilijua hakuna aliyeanza chuo cha mahusiano ya ndoa aliyemaliza kozi na kufika mwisho wa kujifunza kabla hajafa.
Tuendelee kujifunza na kusaidiana kupeana uzoefu maana hii ni taasisi pana na haina mwisho. ASANTENI na toa mawazo yako pia katika kipengele cha COMMENTS. Busara itumike wakati wa kutoa COMMENTS.
Sunday, June 5, 2016
MAHUSIANO
_1.Ule usemi kuwa wanaume wa Dar wanakula chips mayai badala ya ugali wa dona kuwa ni chanzo cha migogoro ktk mahusiano kwa wapenzi wao HUENDA IKAWA SIO KWELI kwa kuzingatia kanuni za lishe bora ni ipi.....
_2.Uzuri wa sura,rangi au umbo eti ni kipaumbele katika mahusiano......pia sio kweli kwa mujibu wa uzoefu...
Nionavyo mimi
Wazo zuri la ugali wa dona,lakini sizani kama ugali ndio tatizo pekee,maana hata ughaibuni hawali dona na mahusiano yao yako Juu. Lishe ni mhimu lakini haisababishi mahusiano yawe bora pasipokujua virutubisho vya mahusiano. *Illiterate* wa mahusiano anaweza kuwa mme au mke, ugal hatukatai bali ifahamike hiyo siyo mechi ya _simba na yanga_ ni zaidi ya kutumika kwa *energy* kama tafsiri ya ugali ilivyo.
Partners can be all *energetic enough* for the marathon yet can not achieve the satisfaction point " *climax*" . partners used to ignore _sex education_ , pretending to know more than what the truth counts.
Mfumo rasmi wa Elimu hauna somo la mahusiano,ni jukumu la mhitaji kutafuta ujuzi na maarifa nje ya mfumo rasmi.
Bahati mbaya wasomi wengi ni waathirika wa mambo haya sababu wanajiona wanajua kumbe hawajui. Mapenzi hayana cha _prof,Dr wala kilaza_, na ni bora kujifanya huyajui ili utafute kujua.
*SATISFACTION* ??
Swali linakuwa
_how do I satisfy him/her_ ?
_how do I know that he/she is sexually satisfied_ ?
_does satisfaction refers to bed sex alone_?
_do partners knows all about intimacy_?
Sumu ya mahusiano ni jambo la kufahamu pia. Wapendanao waachane na *kiburi,ubabe,ukatili,dharau,ujuaji usio na tija,utapeli,usaliti,uongo,udanganyifu,ulaghai,aibu,woga,uchafu,umaskini,uvivu,uzembe, tafsiri potoshaji za kidini n.k* siwezi taja yote mengine yanategemea matakwa ya wapendanao _e.g sigara,ulevi,wizi,ujambazi,ushirkina,uchawi,uporaji,ugomvi,n.k_ haya yanategemeana na wapendanao.
2. Ikumbukwe uzuri wa sura,rangi au umbo la mwanamme/mwanamke ni sehemu ndogo sana katika suala zima la utosherevu wa kimahusiano, ni vigezo vidogo sana kati ya vingi vingine. Laiti ingekuwa hivyo bilashaka warembo walioko baa ( *bar-made* ) wangekuwa wameolewa sababu wanasifa zote kwa mwonekano wa nje, WANAMVUTO WA SURA NA SHEPU....
Wengi wameharibu mahusiano yao kwa kuwalinganisha wapenzi wao na wale wa kwenye mitandao ya kijamii,au kutaka wapenzi wao wafanye au kuiga kama yaonekanayo ktk mitandao. Sidhani kama ni vizuri kutaka mwenzi aonekane au kufanana na kila sifa ya uzuri ionekanayo ktk mitandao, Mungu hakutuumba wote sawa kwa sura,rangi wala maumbo. Hata hivyo hayo yananafasi Ndogo sana ktk mahusiano.
Tusisahau, hakuna mbabe wa mapenzi. Ni bahari pana na kila mtu anaogelea kwa kadri awezavyo kupiga mbizi. Tujifunze tusiridhike na elimu ndogo ya mahusiano tuliyonayo. Tujitahidi kuyajua mahusiano kwa mapana yake.
👩❤️👩. 👫. 💃🏃🏻
Mungu atuwezeshe kujua yale tusiyoyajua.
Mimi sio mtaalamu sana niache uwanja wazi wengine watasema zaidi.
Monday, May 30, 2016
MATAPELI WA FACEBOOK
Kuna wimbi kubwa la matapeli wa mitandaoni. Wengi wao hutumia majina feki,picha feki na baadhi ya vitu vya jinsi hiyo.
Facebook imekuwa kinara wa tatizo hili pia. Nimependa makala hii ( bonyeza hapa ) itakusaidia pia.
Friday, June 19, 2015
Tufuate ushauri wa madaktari.
Habari za Leo tena ndungu zangu wapendwa. Ni Siku nyingine nzuri Mungu ametupa tupate kufurahia maisha pamoja na changamoto same.
Leo naomba kuzungumzia changamoto moja ambayo imewapata watu wengi,inawezekana hata wewe umewahi kupitia changamoto hii. Kuna hili suala la maduka ya madawa ya dawa muhimu za binadamu, maarufu kama dawa baridi. Wengi wetu tumezoea njia za mkato,tunaenda kupata dawa huko bila ushauri wa daktari. Tujiulize je! Wale wahudumu wa dukani wanaelimu ya pharmacist?? Ukweli unao. Mbaya zaidi tunalizika kuandikiwa kanywe 2×3 na tunalizika bila kujua madhara ya Dawa hizo. Ikumbukwe kuwa kila dawa ni sumu isipotumika kwa utaratibu unaotakiwa.
Unakuta mhudumu anamwuliza mteja, unataka za nchi gani? Au eti Mimi ninazo za India na Italia wewe unataka ipi? Jamani hivi raia wa kawaida anafahamu description ya dawa hizi pamoja na ubora wa viwanda vyake? Bilashaka sheria inawataka wamiriki wa maduka hayo waajiri watu wenye ujuzi wa madawa na sio vinginevyo. Tatizo unakuta mmiriki kaweka ndugu take darasa la saba au kidato cha nne, wengine wanaelimu ya nursing hata hao nao sheria hairuhusu wao kuchukua nafasi ya daktari. Unakuta mteja anatoa maelezo dukani ya ugonjwa wake baada ya maelezo wale wauzaji wanatumia uzoefu wao kumpatia mgonjwa dawa. Mwisho wa siku tunalalamika ongezeko la cancer katika jumuia zetu,vifo vingi kwa ugonjwa mdogo ambao unatibika.
Wengine wamegeuza maduka kuwa vituo vya afya. Mfano wanaotoa huduma ya kuchomwa sindano dukani, kuoshwa na kufunga vidonda nk je sheria inaruhusu? Najaribu kutafakari sana kuwa wengi wanaomiriki haya maduka ni watu wanaotoa huduma au waajiriwa katika hospitali zilizosajiliwa na wanafahamu masharti ya kuanzisha duka la dawa baridi. Kwa nini hawazingatii ni swali langu kwa mamlaka zinazohusika kutoa leseni za biashara hizo,labda wanamaelezo ya ziada. Naamini mamlaka hizo pia zinafanya kazi vizuri lakini bado raia nao wanatakiwa kujifunza juu ya hili wafuate ushauri wa daktari kabla hawajaenda kununua Dawa dukani. Kama tatizo ni elimu juu ya hatari ya matumizi mabaya ya dawa hizi za binadamu basi tuziombe mamlaka husika zisaidie kuelimisha wananchi mara kwa mara.
Yangu leo ni hayo machache niwatakie ushirikiano mzuri wa Elimu ya hatari za matumizi mabaya ya Dawa za binadamu ili watu wengi wapate ufahamu wa kutosha. Tusaidiane kuelimishana ili kuokoa maisha ya wengi. Asante kwa kufuatilia makala hii.
Saturday, June 13, 2015
TUFANYE KAZI KWA BIDII
Habari za w/end, nawatakia mapumziko mazuri. Kule ukweni Dubai w/end mwisho ufukwe wa bahari Hindi,ukikanyaga nchi kavu kila mtu bize,
But kwetu tunalala w/end eti mapumziko,zen tunasema maisha magumu. Halafu nyie wenye ndoa zenu ndo kabisaaaaa.....! Think twice,
Angalia budget ya nchi ya 2015/2016 ni tegemezi, swali langu ni kwanini tuwategemee wenzetu kila mwaka sisi hatuwezi badilika? Tunajifanya mafundi wa kuimalisha ndoa,samahani kama utachukia BT huo ni ukweli bongo tumezidi uzembe,tumeona suluhu in kuongeza kodi kwenye petrol,diesel,kerosene,magari nk halafu tumeacha pombe na vileo vyote viwe na bei poa ili tuendekeze ulevi na uvivu wa kufikili???
Hadi mkulima kijijini ameambukizea ugonjwa wa w/end, nani kasema upumzike still unakalia kigoda, !!!
TANZANIA NAKUPENDA ILA FIKIRA ZAKO ZINANICHOSHA. UNANIAHIDI NIISHI KWA MATUMAINI NISIYOYATARAJIA KUYAPATA LEO WALA KESHO.
Bajeti iliyowasilishwa imenitafakarisha sana,I wish wanaojinadi urais mwaka huu wangeonesha kuipinga hiyo bajeti tuwaamini kuwa kweli wanatuingiza kwenye matumaini mazuri, bt nothing spoken from their mouths,!!!!
Real wonders will never end..,..!!!!!
Let us work men.
Sunday, July 29, 2012
MGOMO WA WALIMU TANZANIA.
Hatimaye chama cha walimu Tanzania ( CWT ) kimethibitisha kuwa mgomo wa walimu nchi nzima uko palepale kuanzia jumatatu tarehe 31-julai-2012. Rais wa CWT, Gratian Mukoba ameitaka serikali kuacha vitisho dhidi ya walimu. Aidha mgomo huo utakuwa halali baada ya serikali kupewa notisi ya saa 48 iliyoanza saa 8 mchana ijumaa na kuisha saa 8 mchana jumapili kisha kutangaza rasmi mgomo huo kuanzia jumatatu.
Madai ya walimu ni pamoja na ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55, asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya sanaa na posho kwa walimu wanaoishi katika mazingira magumu.
Kwa mujibu wa chapisho la gazeti la Mwananchi la tarehe 29-7-2012, kauli ya Wizara kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipoulizwa kuhusu uamuzi wa walimu kuendelea na mgomo, alisema hawezi kuzungumzia hilo yuko safarini kuelekea Mbeya.
“Siwezi kuzungumza nipo safarini kuelekea Mbeya na hatuwezi kuelewana hivyo, mtafute Waziri atazungumzia,” alisema Mulugo.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipopigiwa simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokewa.
Kutokana na gharama za maisha kuwa ngumu kw watanzania wa kipato cha chini, ni dhahiri kuwa kuna umuhimu kwa walimu kusikirizwa madai yao. Hata waheshimiwa wabunge walikiri kuwa hali ya maisha ni ngumu, lakini walighubikwa na ubinafsi pali waliposema kuwa gharama za maisha mjini Dodoma ni kubwa hivyo wao waongezewe posho. Kama Dodoma maisha ni magumu, je! watanzania wengine waishio hapo Dodoma na mikoa mingine wao nani atawanusuru na hii hali ya maisha magumu? Tunaomba Serikali itambue kuwa hata watumishi wengine wa uma kama walimu, polisi, wauguzi, n. k. wanahitaji kuboreshewa mishahara yao ili kukabiliana na mfumuko wa gharama za maisha.
Madai ya walimu ni pamoja na ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55, asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya sanaa na posho kwa walimu wanaoishi katika mazingira magumu.
Kwa mujibu wa chapisho la gazeti la Mwananchi la tarehe 29-7-2012, kauli ya Wizara kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipoulizwa kuhusu uamuzi wa walimu kuendelea na mgomo, alisema hawezi kuzungumzia hilo yuko safarini kuelekea Mbeya.
“Siwezi kuzungumza nipo safarini kuelekea Mbeya na hatuwezi kuelewana hivyo, mtafute Waziri atazungumzia,” alisema Mulugo.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipopigiwa simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokewa.
Kutokana na gharama za maisha kuwa ngumu kw watanzania wa kipato cha chini, ni dhahiri kuwa kuna umuhimu kwa walimu kusikirizwa madai yao. Hata waheshimiwa wabunge walikiri kuwa hali ya maisha ni ngumu, lakini walighubikwa na ubinafsi pali waliposema kuwa gharama za maisha mjini Dodoma ni kubwa hivyo wao waongezewe posho. Kama Dodoma maisha ni magumu, je! watanzania wengine waishio hapo Dodoma na mikoa mingine wao nani atawanusuru na hii hali ya maisha magumu? Tunaomba Serikali itambue kuwa hata watumishi wengine wa uma kama walimu, polisi, wauguzi, n. k. wanahitaji kuboreshewa mishahara yao ili kukabiliana na mfumuko wa gharama za maisha.
Friday, April 6, 2012
Kwaheri Bingu wa Mutharika, Malawi
Hatimaye aliyekuwa raisi wa Malawi, Bingu wa Mutharika inasemekana amefariki dunia huko afrika ya kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo. Poleni sana wananchi wote wa Malawi tunawaombea amani na utulivu katika kipindi hiki kigumu cha kusubiri atakayerithi nyayo za Mutharika.
Habari zaidi kutoka BBC NEWS
One of the doctors who treated Mr Mutharika, 78, said the president was "clinically dead" on Thursday after suffering a cardiac arrest.
State media has only reported that he has been flown to South Africa for medical treatment.
If confirmed, his death would spark a constitutional crisis, analysts say.
According to the constitution, the vice-president takes over if the head of state is incapacitated or dies in office.
But Vice-President Joyce Banda and Mr Mutharika fell out after a row over the succession in 2010, and she was expelled from the ruling Democratic People's Party (DPP).
Mr Mutharika's brother, Foreign Minister Peter Mutharika, was chosen instead of Ms Banda to be the DPP's presidential candidate in the 2014 elections.
The doctors and ministers say that Mr Mutharika's body was taken to South Africa while a decision is taken about what to do next.
Government sources have told the BBC that efforts to resuscitate President Mutharika had failed and that an official announcement is being prepared.
'The laws are clear' Former President Bakili Muluzi - a bitter rival to Mr Mutharika - has called on the authorities to make an announcement.
"It's important that the government announces the condition of the president as soon as possible so that the nation is informed," he told journalists.
Mr Mutharika, a former World Bank economist, came to power in a 2004 election, after being backed by outgoing President Muluzi. Soon afterwards, Mr Mutharika left his United Democratic Front (UDF) to form the DPP, after accusing Mr Muluzi and other UDF leaders of opposing his campaign against corruption.
Since being re-elected with a large majority in 2009, critics allege he has demonstrated an increasingly authoritarian streak.
The president has been under mounting pressure to resign, amid accusations of nepotism and economic mismanagement.
The criticism has led to a souring in relations with major foreign aid donors, especially the United Kingdom.
Last year, Mr Mutharika expelled the UK High Commissioner, Fergus Cochrane-Dyet, after a leaked embassy cable quoted the diplomat as saying that the president could not tolerate criticism.
The Malawian leader said he could not accept "insults" just because the UK was his country's largest aid donor.
In response, the UK expelled the Malawian envoy to London and cut direct aid.
Malawi is one of the poorest countries in the world, with an estimated 75% of the population living on less than $1 (60p) a day.
The country has suffered shortages of fuel and foreign currency since the UK and other donors cancelled aid.
Kwa habari zaidi someni:
http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-17636393
http://news.yahoo.com/malawi-president-dies-heart-attack-hospital-075230249.html
Habari zaidi kutoka BBC NEWS
Malawi President Bingu wa Mutharika 'dead'
President Bingu wa Mutharika of Malawi has died, doctors and cabinet ministers have told the BBC, but this has not been officially announced.
State media has only reported that he has been flown to South Africa for medical treatment.
If confirmed, his death would spark a constitutional crisis, analysts say.
According to the constitution, the vice-president takes over if the head of state is incapacitated or dies in office.
But Vice-President Joyce Banda and Mr Mutharika fell out after a row over the succession in 2010, and she was expelled from the ruling Democratic People's Party (DPP).
Mr Mutharika's brother, Foreign Minister Peter Mutharika, was chosen instead of Ms Banda to be the DPP's presidential candidate in the 2014 elections.
He has been standing in for the president when needed during official occasions. Ms Banda recently told the BBC she had not spoken to Bingu wa Mutharika for more than a year.
The BBC's Raphael Tenthani in the main city, Blantyre, says ministers met all night to discuss the situation.The doctors and ministers say that Mr Mutharika's body was taken to South Africa while a decision is taken about what to do next.
Government sources have told the BBC that efforts to resuscitate President Mutharika had failed and that an official announcement is being prepared.
'The laws are clear' Former President Bakili Muluzi - a bitter rival to Mr Mutharika - has called on the authorities to make an announcement.
"It's important that the government announces the condition of the president as soon as possible so that the nation is informed," he told journalists.
"I am calling for a constitutional order, for continued peace and order. The laws of Malawi are very clear that the vice-president takes over when the president can no longer govern."
Since being re-elected with a large majority in 2009, critics allege he has demonstrated an increasingly authoritarian streak.
The president has been under mounting pressure to resign, amid accusations of nepotism and economic mismanagement.
The criticism has led to a souring in relations with major foreign aid donors, especially the United Kingdom.
Last year, Mr Mutharika expelled the UK High Commissioner, Fergus Cochrane-Dyet, after a leaked embassy cable quoted the diplomat as saying that the president could not tolerate criticism.
The Malawian leader said he could not accept "insults" just because the UK was his country's largest aid donor.
In response, the UK expelled the Malawian envoy to London and cut direct aid.
Malawi is one of the poorest countries in the world, with an estimated 75% of the population living on less than $1 (60p) a day.
The country has suffered shortages of fuel and foreign currency since the UK and other donors cancelled aid.
Kwa habari zaidi someni:
http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-17636393
http://news.yahoo.com/malawi-president-dies-heart-attack-hospital-075230249.html
Sunday, September 11, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)