Sunday, December 9, 2018

USHIRIKI WA KAZI ZA ZIADA KWA WANAFUNZI

Kazi kubwa kwa Mwanafunzi shuleni ni kujifunza kulingana na mihutasari iliyowekwa na Wizara ya Elimu. Pamoja na hili jukumu muhimu pia Mwanafunzi anatakiwa ajihusishe na kazi za ziada kama kufanya usafi katika mazingira ya shule, kushiriki kazi za elimu ya kujitegemea na kujiunga na clubs mbalimbali kama FEMA, MALI HAI, SUBJECTS CLUBS, PCCB CLUB, SCOUT na zinginezo nyingi. Mwanafunzi anapojihusisha na hizo kazi za ziada nje ya darasa zinamjenga katika kujitambua zaidi na kuwa raia mwenye kuwajibika katika maisha yake. Hali hiyo humpa muda wa kushirikiana na wenzake na kuwa na mtazamo chanya katika kazi za kizalendo za kujenga Taifa.
Kwa hisani ya Nkoasenga Sekondari, ARUSHA

No comments: