Watanzania tuwe na moyo wa kupenda kutumia nafasi yetu kumpigia kura kiongozi ambaye atatuletea mafanikio kwa kujali na kusikiliza mahitaji ya wananchi. Tusikae nyumbani siku ya kupiga kura tukitegemea kuwakilishwa na wenzetu. Uzarendo wetu kama watanzania uonekane kesho katika vituo vya kupigia kura.
Tukumbuke kuombea nchi yetu tupate kiongozi BORA NA MWADILIFU, nawapa pole sana wanafunzi wa vyuo vikuu ambao mmeshindwa kufanikisha zoezi la kufika katika vituo vyenu vya kupigia kura. Tumieni nafasi hii kuwatakia kila la heri wale waliofika katika vituo vyao kutimiza haki yao ya kikatiba.