Jamani narudi tena katika ulingo huu wa wanaopenda kusemasema, maana hata mtembea bure si sawa na mkaa bure......japo siku moja nilikuwa juu ya mawe.."bankrupt" nikakumbuka usemi huu nikatoka nyumbani kwenda kutembea nikiwa na tumaini la kupata chochote, sikuona huo muujiza. Rafiki yangu kuna misemo mingine ya kiswahili inaweza kukuingiza chaka.
Naomba uchanganuzi wa maneno haya ambayo yanatumiwa sana na watanzania wengi.
- mtu akisema BONGO anamaana sawa na jina la nchi, yaani TANZANIA?
- nini wingi wa neno UBONGO?
- Je! kuna uhusiano wowote wa kilugha kati ya neno BONGO na UBONGO? eleza kidogo.
- wengi husema ukiishi bongo lazima uchangamshe ubongo maana bongo ni kwa wajanja tu....! kuna uhusiano wowote wa usemi huu na hali halisi ya watanzania waishio bongo?
Karibu kwenye shamba darasa lisilojali umri wa mtahiniwa.......elimu ni bahari.
No comments:
Post a Comment