Sunday, December 19, 2010

MKONGWE WA FARISAFA.

Nawasalimuni wote ndugu zangu. Naomba nirejee tena na mada hii ambayo imenipa kufikiri sana bila kupata muafaka wa mawazo yangu. Nimejihisi kuwa labda nimekuwa mvivu wa kusoma maandiko matakatifu ya Mungu.
Yesu anatajwa sana habari zake na hivi karibuni tunaelekea kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwake. Pamoja na jitihada zote za kutaka kufahamu kwa nini Yesu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kujibu maswali yote aliyoulizwa, nimekosa habari zake muhimu.
  • Yesu mnazareti, aliyezaliwa na Bikira Mariam, alisoma shule gani na chuo kipi?
  • Naomba kujua kiwango chake cha elimu.
Makuhani, Maliwali, Mafarisayo na wasomi wengine waliuliza maswali mengi kutaka kumtega, lakini Yesu alikuwa na uwezo wa kutoa hadi "reference" kwa kusema " IMEANDIKWA". Hata nyoka alipotaka kumjaribu Yesu, alijibu "IMEANDIKWA usimjaribu Bwana Mungu wako"
  • Kwa nini walimwita Mwalimu hata wasomi waliokuwa na elimu ya juu katika Uyahudi?

"NAWATAKIA CHISTMAS NJEMA NA HERI YA MWAKA MPYA 2011"

Friday, December 17, 2010

BIDHAA FEKI

Mfumo wa elimu Tanzania umejikita zaidi katika masomo ya nadharia kuliko vitendo. hali hii imetuathiri sana wananchi kwa sababu wengi wetu hatuna ubunifu wa kutosha wa kumudu ushindani wa soko la leo duniani. Ukipita mtaani utajionea bidhaa nyingi zijulikanazo kwa jina la 'MCHINA' zikiwa zimesambaa kila kona. Ukitafuta uwiano na kile tunachozalisha sisi dhahili utagundua tofauti kubwa.
Bidhaa za kigeni.

Viwanda vyetu viko wapi hadi tumevamiwa na bidhaa toka ughaibuni na kuziba vya kwetu?. Tusaidieni enyi watanzania mlioko nchini China, Japani, Korea, India kama huko mitaani kuna bidhaa zetu za kitanzania zinazouzwa zikiwa na nembo ya TBS na chata ya MADE IN TANZANIA.
Kaulimbiu ya nchi inasema 'KILIMO KWANZA' lakini ukienda shopright utakutana na bidhaa kama apple, coffee, milk, juice, onions, na matunda mengi kutoka nchi za nje kama Afrika kusini, kwa nini tusijivunie na vya kwetu? hii kaulimbiu ni ya majukwaani tu?
 
Haya nayo lazima yatoke nje?
Nafikiri ni vyema zaidi kama sera za uzalishaji mali na ukuaji wa viwanda za nchi zingetoa kipau mbele katika kukuza soko la bidhaa zetu asilia. Hata kama zitaonekana kuwa sio bora kama za wenzetu hapo ndipo tutajua jinsi ya kurekebisha na kukidhi mahitaji ya ushindani katika masoko yetu na ya nje.

Wednesday, November 24, 2010

MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI 2010

Rais Jakaya Kikwete akitangaza baraza jipya la Mawaziri leo Ikulu jijini Dar es salaam

1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe

2. Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu:  Stephen Wassira
3.Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
4. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano):  Samia Suluhu
5. . Ofisi ya  Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
7.  Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
9. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
Naibu: Pereira Ame Silima
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
17. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
18. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
19. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
20. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
21. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
24. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu:Dr. Fenella Mukangara
27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge

Hiyo ndo serikali iliyokuwa ikisubiliwa kwa shauku kubwa na Watanzania.

Monday, November 22, 2010

KIJIWENI

Mara nyingi ukipita mtaani kwenye vijiwe vya wazee wapenda kahawa utasikia jinsi wanavyotumia muda wao mwingi kupanga safu ya Baraza la mawaziri la serikali ya Kikwete. Mimi nafikiri wangetumia muda huo kujadili mipango bunifu ya kuweza kufanyika katika serikali zao za mitaa ili kijiletea manufaa zaidi.
Maranyingi tumekuwa tukipoteza muda mwingi kufanya kazi za watu katika dhana ya kusadikika na mwisho wa siku hujikuta tumechelewa kutekeleza majukumu yetu muhimu.

Thursday, November 11, 2010

SPIKA WA BUNGE

Hatimaye mambo ya uchaguzi yamepita na sasa kizaza kingine ni juu ya upatikanaji wa spika wa Bunge letu. Hadi sasa kuna mizengwe mingi bado inaendelea katika mchakato wa waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Nimebaki njia panda kwani sijawa na ushahidi wa kutosha kumhusu mheshimiwa Samwel Sita, amekuwa akipingwa sana na wanaCCM kuwa asipewe tena nafasi hiyo. Tunaomba waweke wazi vipingamizi vyao vina sababu za msingi?
Samwel Sitta

Baadhi ya tuhuma zake zinasema Ujue ufisadi wa samwel sita.
Lakini hayo ni kweli?

Sunday, October 31, 2010

RAISI MPYA TZ.

Ni siku nzuri ambayo watanzania tunatimiza haki yetu ya kikatiba na bado masaa machache sasa tufikie hatima ya kuwa na raisi mpya. Nimeamka alfajiri na mapema kuwahi kituoni. Niwapongeze wananchi kwa moyo wa kutekeleza haki yenu na ninaamini mwamko huu utasaidia sana kufikia malengo mazuri.
Baadhi ya vituo vimeripotiwa kuwa na kasoro ndogondogo na kwa ujumla hali ni shwari katika vituo vingi. Tutulize mawazo tusubili majibu ya kura zetu.
Unauwezo wa kutabili nani atakuwa RAISI wako masaa machache yajoyo? BONYEZA HAPA

Saturday, October 30, 2010

UANACHAMA BILA KUPIGA KURA.


Watanzania tuwe na moyo wa kupenda kutumia nafasi yetu kumpigia kura kiongozi ambaye atatuletea mafanikio kwa kujali na kusikiliza mahitaji ya wananchi. Tusikae nyumbani siku ya kupiga kura tukitegemea kuwakilishwa na wenzetu. Uzarendo wetu kama watanzania uonekane kesho katika vituo vya  kupigia kura.
Tukumbuke kuombea nchi yetu tupate kiongozi BORA NA MWADILIFU, nawapa pole sana wanafunzi wa vyuo vikuu ambao mmeshindwa kufanikisha zoezi la kufika katika vituo vyenu vya kupigia kura. Tumieni nafasi hii kuwatakia kila la heri wale waliofika katika vituo vyao kutimiza haki yao ya kikatiba.

Monday, October 11, 2010

KIDATO CHA NNE 2010.

Nawapa hongera wote kwa kumaliza kidato cha nne. Jiandaeni na maisha ya mtaani. A-Level Schools are very few in Tanzania, get prepared to face life challenges.

You had long journey of four years, but that is just the begining, CONGRATULATIONS

Wednesday, September 15, 2010

Life after college

Mara nyingi maisha baada ya chuo huwa magumu kwa baadhi ya wahitimu. Hili tatizo huja pale mhitimu anapokuwa amejipangia malengo yake ya kimaisha lakini mwajiri wake hugeuka kuwa mbogo mahali pa kazi.

Kumekuwa na manyanyaso mengi katika vituo vingi kwa watumishi pale wakuu wa vituo wanapowabana wahitimu wengi kukosa nafasi za kuhudhuria semina mbalimbali za watumishi, kuishi ndani ya kituo bila kupata nafasi ya kwenda nje ya kituo. Wasiwasi wa wakuu wengi kuogopa kuporwa madaraka yao na watumishi katika vituo vyao waliojiendeleza limekuwa tatizo mojawapo linalofanya waishi kwa shida.
Wahitimu wengi kutoka vyuo vikuu hujikuta hawatimizi malengo yao na mazingira ya kazi kuzidi kuwa magumu kwao. Swali linabaki kwa hawa wakuu wa vituo vya taasisi mbalimbali kuwa kwa nini wasitumie muda wao kujiendeleza kielimu badala ya kuendelea kugombana na watumishi?

Wednesday, August 11, 2010

BONGO.......!

Jamani narudi tena katika ulingo huu wa wanaopenda kusemasema, maana hata mtembea bure si sawa na mkaa bure......japo siku moja nilikuwa juu ya mawe.."bankrupt" nikakumbuka usemi huu nikatoka nyumbani kwenda kutembea nikiwa na tumaini la kupata chochote, sikuona huo muujiza. Rafiki yangu kuna misemo mingine ya kiswahili inaweza kukuingiza chaka.

Naomba uchanganuzi wa maneno haya ambayo yanatumiwa sana na watanzania wengi.
  • mtu akisema BONGO anamaana sawa na jina la nchi, yaani TANZANIA?
  • nini wingi wa neno UBONGO?
  • Je! kuna uhusiano wowote wa kilugha kati ya neno BONGO na UBONGO? eleza kidogo.
  • wengi husema ukiishi bongo lazima uchangamshe ubongo maana bongo ni kwa wajanja tu....! kuna uhusiano wowote wa usemi huu na hali halisi ya watanzania waishio bongo?
 Karibu kwenye shamba darasa lisilojali umri wa mtahiniwa.......elimu ni bahari.

ELIMU YETU.


Ni takribani miaka 40 sasa tangu tupate uhuru Tanzania. Sekta ya elimu imepiga hatua nyingi ikiwemo kaulimbiu ya ujenzi wa shule za kata. Changamoto nazo zimepiga hatua sambamba na wingi wa shule.
Inasikitisha kuona bado idadi kadhaa ya wanafunzi wa shule za sekondari wanakaa chini wakati wa kufundishwa na hata wakati wa mitihani yao. Kwa hali hii ufaulu wa wanafunzi utaongezeka? kwa nini wanafunzi wakifeli jamii inamtazama mwalimu kama chanzo cha tatizo? Ikumbukwe kwamba kuna mambo mengi yanayoweza kuchangia mwanafunzi kufaulu, sio juhudi ya mwalimu pekeyake.
Nchi yetu inautajiri wa kutosha kama madini, mbuga za wanyama, uvuvi, kilimo, misitu nk. Hazina hii inatosha kuboresha uchumi bila kusahau sekta ya elimu. Tuna wasomi wengi na watalamu ndani na nje ya nchi, wakipewa nafasi katika uboreshaji wa elimu tutapiga hatua zaidi.
Sasa ni wakati wa kampeni za uchaguzi wa madiwani, wabunge na uraisi. Je! wagombea watatoa sera gani katika kuinua kiwango cha elimu? Tafiti nyingi za elimu zimefanywa zikiwa na mapendekezo mengi juu ya njia mbadala za kuboresha elimu yetu, matokeo yake tafiti hizi zinarundikana kwenye kabati za taasisi mbalimbali kikiwepo chuo kikuu cha Dar es salaam. Tafiti zimekuwa zikifanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ili kutimiza masharti ya kupa degree, master na PhD……baada ya hapo ‘research reports’ hizi hufungiwa kwenye masanduku.
Hatuwezi kunyoshea kidole mtu Fulani au kikundi cha watu, bali Watanzania wote tuamke na kupiga vita hali duni ya elimu katika nchi yetu. 
Shule hizi za kata zitakuwa na mafanikio kama watoto wote wa viongozi wakuu selikarini  watapeleka watoto wao huko wakachanganyike na watoto wetu kwenye shule zisizo na maabara na uhaba wa walimu.

Thursday, July 22, 2010

VUVUZELA IMEANZA ENZI ZIPI?



Historia inasemaje?


Kumekuwa na maswali mengi kuhusu asili au chanzo cha vuvuzela , chombo kilichotumika kama sehemu ya burudani hivi karibuni huko bondeni. Je! unajua chimbuko lake au hawa wanasingiziwa tu? kama itakuwa kweli unajifunza nini ?
Je! hii inakamilisha usemi usemao "USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA"

Tuesday, July 13, 2010

Ngoma zetu.

Historia inaonesha babu na bibi zetu walikuwa na utamaduni asilia, lakini kizazi cha leo kimebebwa na mitindo ya utamaduni wa kigeni. Bila shaka maamuzi ya kizazi kipya kama miziki yao inavyojitambulisha yalikuwa sahihi kutokana na sabubu walizoziona wao.

Ukiangalia kipande hiki cha ngoma asilia ijulikanayo kama "acrobatic snake dance" utaona radha tofauti na ubora wa tamaduni za wahenga wetu. Ngoma au utamaduni wetu wa asili ulikuwa unatukumbusha mambo mengi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiimani na hata kutuelimisha kisaikolojia. Utamaduni wa kigeni kutoka "ughaibuni" una radha tofauti na isiyokidhi hali halisia ya mazingira yetu tulolisishwa na babu zetu.


Utandawazi unatuweka sote kama kijiji kimoja lakini swali lakujiuliza ni kuangushwa kwa utamaduni wetu wa kiafrika na kujikuta tunakuwa na utandawazi ulojaa sura moja ya vionjo vya kiutamaduni.
Mimi nafikiri tuige mfano wa kaa (au crab) anayejongea kwa kwenda mbele na nyuma pia. Tusisahau tutokako japo kuna umhimu wa kutazama tuendako. Mtu huenda akawa si jasiri sana kama hajiamini au hawezi kujivunia hata kile kidogo alichonacho. MUNGU KATUJALIA MAMBO MENGI WAAFRIKA TUJIAMINI NA TUULINDE UTAMADUNI WETU.

Monday, July 12, 2010

Karibuni ndugu!

Nawakaribisha kwenye kibaraza hiki, nikiwa mgeni kidogo, natambua umuhimu wa kubadilishana mawazo kuelimisha na kuburudisha kuwa ndio msingi mkubwa wa IT. Kwa kiasi nategemea uwepo wenu mtandaoni uwe na msaada kwa wanaoanza na sio kuwa na mtazamo wa kujuana. Karibuni sana