Mfumo wa elimu Tanzania umejikita zaidi katika masomo ya nadharia kuliko vitendo. hali hii imetuathiri sana wananchi kwa sababu wengi wetu hatuna ubunifu wa kutosha wa kumudu ushindani wa soko la leo duniani. Ukipita mtaani utajionea bidhaa nyingi zijulikanazo kwa jina la 'MCHINA' zikiwa zimesambaa kila kona. Ukitafuta uwiano na kile tunachozalisha sisi dhahili utagundua tofauti kubwa.
|
Bidhaa za kigeni. |
Viwanda vyetu viko wapi hadi tumevamiwa na bidhaa toka ughaibuni na kuziba vya kwetu?. Tusaidieni enyi watanzania mlioko nchini China, Japani, Korea, India kama huko mitaani kuna bidhaa zetu za kitanzania zinazouzwa zikiwa na nembo ya TBS na chata ya MADE IN TANZANIA.
Kaulimbiu ya nchi inasema 'KILIMO KWANZA' lakini ukienda shopright utakutana na bidhaa kama apple, coffee, milk, juice, onions, na matunda mengi kutoka nchi za nje kama Afrika kusini, kwa nini tusijivunie na vya kwetu? hii kaulimbiu ni ya majukwaani tu?
|
Haya nayo lazima yatoke nje? |
Nafikiri ni vyema zaidi kama sera za uzalishaji mali na ukuaji wa viwanda za nchi zingetoa kipau mbele katika kukuza soko la bidhaa zetu asilia. Hata kama zitaonekana kuwa sio bora kama za wenzetu hapo ndipo tutajua jinsi ya kurekebisha na kukidhi mahitaji ya ushindani katika masoko yetu na ya nje.