Mfumo wa elimu Tanzania umejikita zaidi katika masomo ya nadharia kuliko vitendo. hali hii imetuathiri sana wananchi kwa sababu wengi wetu hatuna ubunifu wa kutosha wa kumudu ushindani wa soko la leo duniani. Ukipita mtaani utajionea bidhaa nyingi zijulikanazo kwa jina la 'MCHINA' zikiwa zimesambaa kila kona. Ukitafuta uwiano na kile tunachozalisha sisi dhahili utagundua tofauti kubwa.
 |
| Bidhaa za kigeni. |
Viwanda vyetu viko wapi hadi tumevamiwa na bidhaa toka ughaibuni na kuziba vya kwetu?. Tusaidieni enyi watanzania mlioko nchini China, Japani, Korea, India kama huko mitaani kuna bidhaa zetu za kitanzania zinazouzwa zikiwa na nembo ya TBS na chata ya MADE IN TANZANIA.
Kaulimbiu ya nchi inasema 'KILIMO KWANZA' lakini ukienda shopright utakutana na bidhaa kama apple, coffee, milk, juice, onions, na matunda mengi kutoka nchi za nje kama Afrika kusini, kwa nini tusijivunie na vya kwetu? hii kaulimbiu ni ya majukwaani tu?
|
| Haya nayo lazima yatoke nje? |
Nafikiri ni vyema zaidi kama sera za uzalishaji mali na ukuaji wa viwanda za nchi zingetoa kipau mbele katika kukuza soko la bidhaa zetu asilia. Hata kama zitaonekana kuwa sio bora kama za wenzetu hapo ndipo tutajua jinsi ya kurekebisha na kukidhi mahitaji ya ushindani katika masoko yetu na ya nje.
3 comments:
Nadhani watanzania tuna kasumba ya kudharau vitu vyetu.
Tazama namna tunavyodharau lugha yetu ya Kiswahili na kutoa kipau mbele kwa lugha za kigeni.
Ni aibu kwetu watanzania, hadi brashi na vichokoleo vya meno vya kichina? Tunahitaji kuwa wazalendo wa kweli!!!
Ni kweli Albert, mimi natumia miba na vipande vya nyasi kuchokolea meno, je! huo nao ni uzalendo?
Ushuhuda Wangu Wa Dhati 💖
Baada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba ndefu, nilivunjika kabisa. Alinifungia kwenye mitandao yote ya kijamii, akasafiri mbali, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Nilikaribia kukata tamaa juu yetu, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitenda.
Siku moja, bosi wangu kazini aliona jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dk. Dk. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu atanirudia ndani ya siku tatu. Kusema kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao mkubwa zaidi, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa ni yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa wenye nguvu na mzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akinipenda na kunijali sana mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa baada ya miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dk. Dawn, ambaye kwa kweli aliwezesha jambo lisilowezekana. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya mahusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Ugumba au matatizo ya bahati nasibu
Kesi za mahakama au kurejesha mali
Dk. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurejesha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
Post a Comment