Friday, June 19, 2015

Tufuate ushauri wa madaktari.

Habari za Leo tena ndungu zangu wapendwa. Ni Siku nyingine nzuri Mungu ametupa tupate kufurahia maisha pamoja na changamoto same. Leo naomba kuzungumzia changamoto moja ambayo imewapata watu wengi,inawezekana hata wewe umewahi kupitia changamoto hii. Kuna hili suala la maduka ya madawa ya dawa muhimu za binadamu, maarufu kama dawa baridi. Wengi wetu tumezoea njia za mkato,tunaenda kupata dawa huko bila ushauri wa daktari. Tujiulize je! Wale wahudumu wa dukani wanaelimu ya pharmacist?? Ukweli unao. Mbaya zaidi tunalizika kuandikiwa kanywe 2×3 na tunalizika bila kujua madhara ya Dawa hizo. Ikumbukwe kuwa kila dawa ni sumu isipotumika kwa utaratibu unaotakiwa. Unakuta mhudumu anamwuliza mteja, unataka za nchi gani? Au eti Mimi ninazo za India na Italia wewe unataka ipi? Jamani hivi raia wa kawaida anafahamu description ya dawa hizi pamoja na ubora wa viwanda vyake? Bilashaka sheria inawataka wamiriki wa maduka hayo waajiri watu wenye ujuzi wa madawa na sio vinginevyo. Tatizo unakuta mmiriki kaweka ndugu take darasa la saba au kidato cha nne, wengine wanaelimu ya nursing hata hao nao sheria hairuhusu wao kuchukua nafasi ya daktari. Unakuta mteja anatoa maelezo dukani ya ugonjwa wake baada ya maelezo wale wauzaji wanatumia uzoefu wao kumpatia mgonjwa dawa. Mwisho wa siku tunalalamika ongezeko la cancer katika jumuia zetu,vifo vingi kwa ugonjwa mdogo ambao unatibika. Wengine wamegeuza maduka kuwa vituo vya afya. Mfano wanaotoa huduma ya kuchomwa sindano dukani, kuoshwa na kufunga vidonda nk je sheria inaruhusu? Najaribu kutafakari sana kuwa wengi wanaomiriki haya maduka ni watu wanaotoa huduma au waajiriwa katika hospitali zilizosajiliwa na wanafahamu masharti ya kuanzisha duka la dawa baridi. Kwa nini hawazingatii ni swali langu kwa mamlaka zinazohusika kutoa leseni za biashara hizo,labda wanamaelezo ya ziada. Naamini mamlaka hizo pia zinafanya kazi vizuri lakini bado raia nao wanatakiwa kujifunza juu ya hili wafuate ushauri wa daktari kabla hawajaenda kununua Dawa dukani. Kama tatizo ni elimu juu ya hatari ya matumizi mabaya ya dawa hizi za binadamu basi tuziombe mamlaka husika zisaidie kuelimisha wananchi mara kwa mara. Yangu leo ni hayo machache niwatakie ushirikiano mzuri wa Elimu ya hatari za matumizi mabaya ya Dawa za binadamu ili watu wengi wapate ufahamu wa kutosha. Tusaidiane kuelimishana ili kuokoa maisha ya wengi. Asante kwa kufuatilia makala hii.

No comments: