Saturday, July 9, 2016

YAJUE MAHUSIANO.

KWA WANAWAKE NA WANAUME WOTE WANAOTARAJIA KUINGIA AU WALIOPO KWENYE NDOA. Nafahamu mlio wengi hampendi kusoma vitabu vinavyotoa Elimu ya mahusiano,mkienda shopping mnaishia kununua nguo,urembo,na chakula cha familia tu wala hamuoni kuwa kuna umhimu wa kupita bookshop upate japo nakala 1 ya kitabu kitakachokupa ujuzi wa kumlea huyo Mke au Mme wako.!! Ikumbukwe kuwa sio vitabu vyote vyaweza kukupa maarifa mazuri bali uchuje kabla ya kutekeleza. Kama lugha ya vitabu vingine itakuwa ngumu ( kingereza ) waweza pia kupata elimu hii kwa njia zingine ndani ya jamii kwa watu wanaojiheshimu na kujali maadili yetu ya kiafrika na misingi ya imani za dini yako. . . Haijalishi ni msomi wa kiwango gani bado kumbuka Elimu ya mahusiano haifundishwi sekondari wala chuokikuu. Hata hao wataalam wa kufunda unyago yawezekana hawajakupa vitu vyote unavyotakiwa kuvitekeleza katika ndoa yako.. . Usiishie tu kujifariji eti unajua,wakati moyo wako unakushuhudia kuwa ndoa yako iko na matatizo. Umekuwa mtu wa kuzunguka kuhudhuria maombezi kwa watumishi wa Mungu bila mafanikio,lazima ujue kuna wajibu wako unatakiwa ufanye kwa vitendo naye Mungu atabariki mahusiano yenu,usiishie kusema namwachia Mungu, hapana.. . *TAFAKALI MAMBO HAYA YATAKUSAIDIA.* . . Ni jukumu lako kuwa romantic kwa mumeo/mkeo. Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi yako kwa mume/mke wako. Mtumie meseji mume/mke wako anapokuwa kazini, muda mwingine hata kama yupo nyumbani mnaangalia TV chati nae katika mitandao ya kijamii (whatsapp, Imo, Facebook etc) hata kama yupo mbele yako jifanye hujui halafu tuma msg nzuri. Hii huleta faraja na ni njia mojawapo ya kuwa romantic kwa mwanaume au mwanamke wako. Jadiliana nae jinsi gani anavyokuvutia. Mnunulie zawadi hata leso, underware, perfume, viatu etc. Mnapokua mezani mkila pamoja labda nyama, mpe nyama kubwa kuliko zote. Tumieni sauti zenu laini kubembelezana na kudekezana, muimbie wimbo mzuri na kutaniana mnapokua pamoja chumbani, acheni u-serious kama mpo kwenye kikao cha bodi ya Korosho,unajifanya kilawakati umekunja sura utazani upo kwenye mkesha wa maombi, loooo !! Aibu. Mume au mke wako anaporudi toka kazini usimkaribishe huku umenuna utafikiri shabiki wa Arsenal aliekosa kombe baada ya msimu wa ligi kuisha. Epuka kuwa mchafu, weka mwili wako msafi pale inapolazimu kama hauko na kazi zinazosababisha uchafu. Jiweke vizuri muonekano na mavazi yako, jua nini uvae na wakati gani.Haijalishi hali ya kiuchumi uliyonayo bali jiweke vizuri kulingana na kile kidogo ulichonacho, usilazimishe maisha ya gharama wakati huna uwezo huo. Mkaribishe mwenza wako kwa kumkumbatia au kwa hali itakayompa amani na furaha, na asubuhi anapoenda kazini Muombee Mungu amwepushe na mabalaa na muombee mafanikio(sio lazima uombe kwa taratibu za kawaida bali mtamkie neno la baraka tu inatosha). Msupport, mshauri, muondoe uchungu, mfariji pale panapokua na matatizo, sio kazi ndogo kuwa mwanaume/mwanamke. Sasa ujinga uliopo kwa baadhi ya wanawake ni kujifanya wako bize na kuwaachia house girls kupokea waume zao watokapo kazini, hivi msichana wa kazi akimpokea mmeo kila siku na labda kinatabia ya kuvaa vibaya nguo unatarajia nini kwa mmeo? Umekaa kujipa matumaini eti Mme wangu mshika dini nani alikudanganya mwili wa mmeo nao umeshika dini !!? Acha uzembe mwanamke. Nanyi wanaume wenye kukaa nje na familia kwa muda mrefu nusu mwaka au mwaka na zaidi eti uko bize kikazi huendi nyumbani kuonana na mkeo, unatengeneza mazingira gani hapo? mbaya zaidi hauko nje ya nchi,unashindwaje kusafiru japo mara chache siku kadhaa unaiona familia unarudi kazini kwako. Mfano mme uko Mtwara na mke yuko Mwanza, kama unajua thamani ya mapenzi yenu lazima tu utakuwa na utaratibu mzuri wa kuchokoka kwenda kumwona mwenzako au mnapanga kukutania mji mwingine kama Dodoma kwa mfano wangu hapo juu ili kurahisisha muonane hata weekend moja kila mwezi inasaidia.Usitengeneze mazingira ya kumuweka mwenza wako katika majaribu ya mahusiano nje ya ndoa, hatusemi kuwa naye karibu ndo dawa ya kutosaliti bali kuna wengine wanasababisha kusalitiwa pia. Pale unapoona anapoteza matumaini ni kazi yako kumpa moyo ni wakati ambao anakuhitaji sana uwe karibu yake na sio kumkwaza tena. Usimfananishe na wanaume au wanawake wengine. Mwanamke mpikie mmeo chakula akipendacho, mfulie nguo zake, mvalishe nguo na mpeti peti akiwa anaumwa. Muamshane asubuhi na mapema, na msilalamikiane kama mmoja wenu anatabia ya kukoroma. Acha Kiss iwe njia yenu ya kuwasiliana wakati mwingine. Soma vitabu kuelewa namna ya kuishi na mume au mke, usijifunze kutoka katika movie. Ya kwenye Muvi Mengi sio ya kweli. Muite mume au mke wako jina lake la utani pia muite jina lake halisi hata kama ni mkubwa sana kuliko wewe as far as he is comfortable with it. Kumbuka Mwenyezi Mungu ameagiza wanawake kuwatii wanaume zao, na wanaume kuwapenda wake zao. Ndoa sio show off bali ni kujitoa kwa moyo wote. Hakuna jambo zuri kwa watu wawili wanaopendana kweli zaidi ya Ndoa na ukiona Mwanaume au mwanamke anasua sua kila ukimueleza suala la Ndoa, ujue huyo hayuko serious na huenda hajakuweka moyoni kuwa naye maisha yenu yote, fungua macho fanya maamuzi kabla hujapotezewa muda wako bila mafanikio ya kuishi naye pamoja. Usilazimishe mapenzi ya kuoa au kuolewa na mtu ambaye hakutaki, soma alama za nyakati na ufanye maamizi sahihi. *msichana ama mwanamke jiepushe na Mambo ya kuweka kinyongo na kulipiza visasi,hasira,kunyimana unyumba,dharau,kujifanya hujui wajibu wake kama mke,kazi zote nyumbani umemwachia house girl,kununa kusiko na maana,kutosikiliza mme wake anataka nini na hupenda nini,unajijali mwenyewe na kadhalika* kinyume na hapo usimlaumu mmeo kukabwa na mchepuko. Michepuko inajua mazaifu ya mke aliyeolewa na ndio maana inaweza kumteka mme wa mtu kiurahisi. Kwa wanaume nao pia wajifunze kujua hisia za mke aliyenaye,kuwa karibu na kutochukulia kiurahisi kila analosema mke, mara nyingi wanawake hawako wazi kwa kila kitu bali hutumia lugha za vitendo na hisia katika kuwasilisha mambo yao, hapa kuna shida na ndoa nyingi zimekwama katika suala la kuijua saikolojia ya mwanamke. Ulimwengu wa kifikra alionao kichwani mwanaume sio lazima ufanane na ulimwengu wa kifikra alionao mwanamke kichwani. Mwanamke anahuruka ya kutaka kutambuliwa kuwa ni MALIKIA PEKEYAKE duniani kote na hakuna malikia mwingine zaidi yake katika wanawake wote duniani na kusikojulikana, hupenda atambuliwe yeye ni malikia anayeweza kila kitu kuanzia jikoni, sebuleni hadi kitandani. Haijalishi uzembe alionao bado atahitaji haki ya kuinuliwa juu kuliko mawingu, wanaume wengi hawako tayari kuona uzembe au madhaifu ya mke halafu wakae kimya bila kukemea na kukalipia,ifahamike kuwa hata MUNGU alisema hawa ni viumbe dhaifu. Na mwanaume au mwanamke ukipata anayejua kukujali,kulea,kukupa raha uitakayo katika maisha yako kwa nini uhangaike na michepuko iliyojaa laana ambayo ni mawakala wa shetani ktk kuvunja taasisi imara ya ndoa iliyoundwa na Mungu mwenyewe? Samahani kwa mwanaume au mwanamke ambaye hujaingia katika maisha ya ndoa, naamini ujumbe huu utakuwa na faida kwako pia baadae Mungu atakapokupa hitaji la moyo wako. Wanaume nao wanawajibu mkubwa kabisa na wanaitwa KICHWA CHA FAMILIA. Lakini wengi wamekuwa sio kichwa kwa mujibu wa kutekeleza majukumu yao katika familia zao, Kila mmoja ajue nafasi yake katika mahusiano na atekeleze bila uzembe maana MAHUSIANO YA NDOA NI TAASISI PANA SANA na haina mtaalamu aliyehitimu na kurizika bali kila mmoja anaishi kwa kumsikiliza mwenzake. Ni taasisi ya Ndoa pekee ambapo wahusika hutunukiwa Vyeti kabla hata hawajaanza kusoma kozi za Chuo kikuu cha Mahusiano. Vyeti hutolewa mapema huenda jamii ilijua hakuna aliyeanza chuo cha mahusiano ya ndoa aliyemaliza kozi na kufika mwisho wa kujifunza kabla hajafa. Tuendelee kujifunza na kusaidiana kupeana uzoefu maana hii ni taasisi pana na haina mwisho. ASANTENI na toa mawazo yako pia katika kipengele cha COMMENTS. Busara itumike wakati wa kutoa COMMENTS.

2 comments:

Unknown said...

Amos Asante sana kwa mada hii maana Naamini ulikuwa na lengo la kufanya iwe msaada kwa mwanamke Lakini kama utakumbukuka tu mume Ni binadamu kamili kabisa utaona kuwa haya yote lazima yatawaliwe na upendo wa kweli na wa dhati. Bila Hilo haijalishi unamkamua kiasi gani asubuhi.

Pia sidhani kuwa kwa kusoma vitabu ndo itapona, maana waandishi wengi wa vitabu anategemea experience zao na sio research.

Kumch Mungu ndio chanzo cha maarifa, sidhani kuwa mkeo wamekuwa mwema kwako kwa kusoma vitabu Bali Ni Hofu ya Mungu ndio imewezesha wewe kuna kuwa Anafaa.

Sio kuwa haifundishi wapo watakaoponywa na hii mada Lakini Hilo sio fundisho la ndo. Tusiache kusoma vitabu Lakini visiwe ndio Msingi wa ufahamu au uelewa wetu pia.

Ndoa Zinatengenezwa na wawili wanaweza kuchagua au kuamua namna iwafaayo.

Asante kwa ujumbe huu

Amos Msengi said...

Asante kwa mawazo mazuri Mdot,ni kweli ndoa ni taasisi ya watu wawili na inahitaji uvimilivu.

Pia haya ni mawazo yanayoweza kusaidia kwa mtu kiboresha mahisiano yake,tusisahau kuwa haya sio mafundisho ya ndoa na yanaweza pia kutofanya kazi kwa baadhi ya watu. Inategemeana na aina ya uelewa wa watu na mazingira wanayopitia katika mahusiano yao.

Mungu siku zote amekuwa msaada kwetu na hajachoka kutusaidia kila tunapomwita. Bali hilo la kumtegemea Mungu halituzuii pia kupata maarifa katika vitabu.

Sio kila kitabu ni kibaya,na pia mtu anapopata mawazo au ushauri katika vitabu lazima achuje kabla ya kutekeleza.

Pia wanaume wakumbuke kuwa wanao wajibu wao mkubwa katika kuyatunza mahusiano na leo sijaongelea hayo ya wanaume.

Nashukuru sana mr. Mdot kwa ushauri wako utasaidia pia. Lengo hapa ni kusaidiana na kupeana uzoefu.