Saturday, July 9, 2016

YAJUE MAHUSIANO.

KWA WANAWAKE NA WANAUME WOTE WANAOTARAJIA KUINGIA AU WALIOPO KWENYE NDOA. Nafahamu mlio wengi hampendi kusoma vitabu vinavyotoa Elimu ya mahusiano,mkienda shopping mnaishia kununua nguo,urembo,na chakula cha familia tu wala hamuoni kuwa kuna umhimu wa kupita bookshop upate japo nakala 1 ya kitabu kitakachokupa ujuzi wa kumlea huyo Mke au Mme wako.!! Ikumbukwe kuwa sio vitabu vyote vyaweza kukupa maarifa mazuri bali uchuje kabla ya kutekeleza. Kama lugha ya vitabu vingine itakuwa ngumu ( kingereza ) waweza pia kupata elimu hii kwa njia zingine ndani ya jamii kwa watu wanaojiheshimu na kujali maadili yetu ya kiafrika na misingi ya imani za dini yako. . . Haijalishi ni msomi wa kiwango gani bado kumbuka Elimu ya mahusiano haifundishwi sekondari wala chuokikuu. Hata hao wataalam wa kufunda unyago yawezekana hawajakupa vitu vyote unavyotakiwa kuvitekeleza katika ndoa yako.. . Usiishie tu kujifariji eti unajua,wakati moyo wako unakushuhudia kuwa ndoa yako iko na matatizo. Umekuwa mtu wa kuzunguka kuhudhuria maombezi kwa watumishi wa Mungu bila mafanikio,lazima ujue kuna wajibu wako unatakiwa ufanye kwa vitendo naye Mungu atabariki mahusiano yenu,usiishie kusema namwachia Mungu, hapana.. . *TAFAKALI MAMBO HAYA YATAKUSAIDIA.* . . Ni jukumu lako kuwa romantic kwa mumeo/mkeo. Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi yako kwa mume/mke wako. Mtumie meseji mume/mke wako anapokuwa kazini, muda mwingine hata kama yupo nyumbani mnaangalia TV chati nae katika mitandao ya kijamii (whatsapp, Imo, Facebook etc) hata kama yupo mbele yako jifanye hujui halafu tuma msg nzuri. Hii huleta faraja na ni njia mojawapo ya kuwa romantic kwa mwanaume au mwanamke wako. Jadiliana nae jinsi gani anavyokuvutia. Mnunulie zawadi hata leso, underware, perfume, viatu etc. Mnapokua mezani mkila pamoja labda nyama, mpe nyama kubwa kuliko zote. Tumieni sauti zenu laini kubembelezana na kudekezana, muimbie wimbo mzuri na kutaniana mnapokua pamoja chumbani, acheni u-serious kama mpo kwenye kikao cha bodi ya Korosho,unajifanya kilawakati umekunja sura utazani upo kwenye mkesha wa maombi, loooo !! Aibu. Mume au mke wako anaporudi toka kazini usimkaribishe huku umenuna utafikiri shabiki wa Arsenal aliekosa kombe baada ya msimu wa ligi kuisha. Epuka kuwa mchafu, weka mwili wako msafi pale inapolazimu kama hauko na kazi zinazosababisha uchafu. Jiweke vizuri muonekano na mavazi yako, jua nini uvae na wakati gani.Haijalishi hali ya kiuchumi uliyonayo bali jiweke vizuri kulingana na kile kidogo ulichonacho, usilazimishe maisha ya gharama wakati huna uwezo huo. Mkaribishe mwenza wako kwa kumkumbatia au kwa hali itakayompa amani na furaha, na asubuhi anapoenda kazini Muombee Mungu amwepushe na mabalaa na muombee mafanikio(sio lazima uombe kwa taratibu za kawaida bali mtamkie neno la baraka tu inatosha). Msupport, mshauri, muondoe uchungu, mfariji pale panapokua na matatizo, sio kazi ndogo kuwa mwanaume/mwanamke. Sasa ujinga uliopo kwa baadhi ya wanawake ni kujifanya wako bize na kuwaachia house girls kupokea waume zao watokapo kazini, hivi msichana wa kazi akimpokea mmeo kila siku na labda kinatabia ya kuvaa vibaya nguo unatarajia nini kwa mmeo? Umekaa kujipa matumaini eti Mme wangu mshika dini nani alikudanganya mwili wa mmeo nao umeshika dini !!? Acha uzembe mwanamke. Nanyi wanaume wenye kukaa nje na familia kwa muda mrefu nusu mwaka au mwaka na zaidi eti uko bize kikazi huendi nyumbani kuonana na mkeo, unatengeneza mazingira gani hapo? mbaya zaidi hauko nje ya nchi,unashindwaje kusafiru japo mara chache siku kadhaa unaiona familia unarudi kazini kwako. Mfano mme uko Mtwara na mke yuko Mwanza, kama unajua thamani ya mapenzi yenu lazima tu utakuwa na utaratibu mzuri wa kuchokoka kwenda kumwona mwenzako au mnapanga kukutania mji mwingine kama Dodoma kwa mfano wangu hapo juu ili kurahisisha muonane hata weekend moja kila mwezi inasaidia.Usitengeneze mazingira ya kumuweka mwenza wako katika majaribu ya mahusiano nje ya ndoa, hatusemi kuwa naye karibu ndo dawa ya kutosaliti bali kuna wengine wanasababisha kusalitiwa pia. Pale unapoona anapoteza matumaini ni kazi yako kumpa moyo ni wakati ambao anakuhitaji sana uwe karibu yake na sio kumkwaza tena. Usimfananishe na wanaume au wanawake wengine. Mwanamke mpikie mmeo chakula akipendacho, mfulie nguo zake, mvalishe nguo na mpeti peti akiwa anaumwa. Muamshane asubuhi na mapema, na msilalamikiane kama mmoja wenu anatabia ya kukoroma. Acha Kiss iwe njia yenu ya kuwasiliana wakati mwingine. Soma vitabu kuelewa namna ya kuishi na mume au mke, usijifunze kutoka katika movie. Ya kwenye Muvi Mengi sio ya kweli. Muite mume au mke wako jina lake la utani pia muite jina lake halisi hata kama ni mkubwa sana kuliko wewe as far as he is comfortable with it. Kumbuka Mwenyezi Mungu ameagiza wanawake kuwatii wanaume zao, na wanaume kuwapenda wake zao. Ndoa sio show off bali ni kujitoa kwa moyo wote. Hakuna jambo zuri kwa watu wawili wanaopendana kweli zaidi ya Ndoa na ukiona Mwanaume au mwanamke anasua sua kila ukimueleza suala la Ndoa, ujue huyo hayuko serious na huenda hajakuweka moyoni kuwa naye maisha yenu yote, fungua macho fanya maamuzi kabla hujapotezewa muda wako bila mafanikio ya kuishi naye pamoja. Usilazimishe mapenzi ya kuoa au kuolewa na mtu ambaye hakutaki, soma alama za nyakati na ufanye maamizi sahihi. *msichana ama mwanamke jiepushe na Mambo ya kuweka kinyongo na kulipiza visasi,hasira,kunyimana unyumba,dharau,kujifanya hujui wajibu wake kama mke,kazi zote nyumbani umemwachia house girl,kununa kusiko na maana,kutosikiliza mme wake anataka nini na hupenda nini,unajijali mwenyewe na kadhalika* kinyume na hapo usimlaumu mmeo kukabwa na mchepuko. Michepuko inajua mazaifu ya mke aliyeolewa na ndio maana inaweza kumteka mme wa mtu kiurahisi. Kwa wanaume nao pia wajifunze kujua hisia za mke aliyenaye,kuwa karibu na kutochukulia kiurahisi kila analosema mke, mara nyingi wanawake hawako wazi kwa kila kitu bali hutumia lugha za vitendo na hisia katika kuwasilisha mambo yao, hapa kuna shida na ndoa nyingi zimekwama katika suala la kuijua saikolojia ya mwanamke. Ulimwengu wa kifikra alionao kichwani mwanaume sio lazima ufanane na ulimwengu wa kifikra alionao mwanamke kichwani. Mwanamke anahuruka ya kutaka kutambuliwa kuwa ni MALIKIA PEKEYAKE duniani kote na hakuna malikia mwingine zaidi yake katika wanawake wote duniani na kusikojulikana, hupenda atambuliwe yeye ni malikia anayeweza kila kitu kuanzia jikoni, sebuleni hadi kitandani. Haijalishi uzembe alionao bado atahitaji haki ya kuinuliwa juu kuliko mawingu, wanaume wengi hawako tayari kuona uzembe au madhaifu ya mke halafu wakae kimya bila kukemea na kukalipia,ifahamike kuwa hata MUNGU alisema hawa ni viumbe dhaifu. Na mwanaume au mwanamke ukipata anayejua kukujali,kulea,kukupa raha uitakayo katika maisha yako kwa nini uhangaike na michepuko iliyojaa laana ambayo ni mawakala wa shetani ktk kuvunja taasisi imara ya ndoa iliyoundwa na Mungu mwenyewe? Samahani kwa mwanaume au mwanamke ambaye hujaingia katika maisha ya ndoa, naamini ujumbe huu utakuwa na faida kwako pia baadae Mungu atakapokupa hitaji la moyo wako. Wanaume nao wanawajibu mkubwa kabisa na wanaitwa KICHWA CHA FAMILIA. Lakini wengi wamekuwa sio kichwa kwa mujibu wa kutekeleza majukumu yao katika familia zao, Kila mmoja ajue nafasi yake katika mahusiano na atekeleze bila uzembe maana MAHUSIANO YA NDOA NI TAASISI PANA SANA na haina mtaalamu aliyehitimu na kurizika bali kila mmoja anaishi kwa kumsikiliza mwenzake. Ni taasisi ya Ndoa pekee ambapo wahusika hutunukiwa Vyeti kabla hata hawajaanza kusoma kozi za Chuo kikuu cha Mahusiano. Vyeti hutolewa mapema huenda jamii ilijua hakuna aliyeanza chuo cha mahusiano ya ndoa aliyemaliza kozi na kufika mwisho wa kujifunza kabla hajafa. Tuendelee kujifunza na kusaidiana kupeana uzoefu maana hii ni taasisi pana na haina mwisho. ASANTENI na toa mawazo yako pia katika kipengele cha COMMENTS. Busara itumike wakati wa kutoa COMMENTS.

Sunday, June 5, 2016

MAHUSIANO

_1.Ule usemi kuwa wanaume wa Dar wanakula chips mayai badala ya ugali wa dona kuwa ni chanzo cha migogoro ktk mahusiano kwa wapenzi wao HUENDA IKAWA SIO KWELI kwa kuzingatia kanuni za lishe bora ni ipi..... _2.Uzuri wa sura,rangi au umbo eti ni kipaumbele katika mahusiano......pia sio kweli kwa mujibu wa uzoefu... Nionavyo mimi Wazo zuri la ugali wa dona,lakini sizani kama ugali ndio tatizo pekee,maana hata ughaibuni hawali dona na mahusiano yao yako Juu. Lishe ni mhimu lakini haisababishi mahusiano yawe bora pasipokujua virutubisho vya mahusiano. *Illiterate* wa mahusiano anaweza kuwa mme au mke, ugal hatukatai bali ifahamike hiyo siyo mechi ya _simba na yanga_ ni zaidi ya kutumika kwa *energy* kama tafsiri ya ugali ilivyo. Partners can be all *energetic enough* for the marathon yet can not achieve the satisfaction point " *climax*" . partners used to ignore _sex education_ , pretending to know more than what the truth counts. Mfumo rasmi wa Elimu hauna somo la mahusiano,ni jukumu la mhitaji kutafuta ujuzi na maarifa nje ya mfumo rasmi. Bahati mbaya wasomi wengi ni waathirika wa mambo haya sababu wanajiona wanajua kumbe hawajui. Mapenzi hayana cha _prof,Dr wala kilaza_, na ni bora kujifanya huyajui ili utafute kujua. *SATISFACTION* ?? Swali linakuwa _how do I satisfy him/her_ ? _how do I know that he/she is sexually satisfied_ ? _does satisfaction refers to bed sex alone_? _do partners knows all about intimacy_? Sumu ya mahusiano ni jambo la kufahamu pia. Wapendanao waachane na *kiburi,ubabe,ukatili,dharau,ujuaji usio na tija,utapeli,usaliti,uongo,udanganyifu,ulaghai,aibu,woga,uchafu,umaskini,uvivu,uzembe, tafsiri potoshaji za kidini n.k* siwezi taja yote mengine yanategemea matakwa ya wapendanao _e.g sigara,ulevi,wizi,ujambazi,ushirkina,uchawi,uporaji,ugomvi,n.k_ haya yanategemeana na wapendanao. 2. Ikumbukwe uzuri wa sura,rangi au umbo la mwanamme/mwanamke ni sehemu ndogo sana katika suala zima la utosherevu wa kimahusiano, ni vigezo vidogo sana kati ya vingi vingine. Laiti ingekuwa hivyo bilashaka warembo walioko baa ( *bar-made* ) wangekuwa wameolewa sababu wanasifa zote kwa mwonekano wa nje, WANAMVUTO WA SURA NA SHEPU.... Wengi wameharibu mahusiano yao kwa kuwalinganisha wapenzi wao na wale wa kwenye mitandao ya kijamii,au kutaka wapenzi wao wafanye au kuiga kama yaonekanayo ktk mitandao. Sidhani kama ni vizuri kutaka mwenzi aonekane au kufanana na kila sifa ya uzuri ionekanayo ktk mitandao, Mungu hakutuumba wote sawa kwa sura,rangi wala maumbo. Hata hivyo hayo yananafasi Ndogo sana ktk mahusiano. Tusisahau, hakuna mbabe wa mapenzi. Ni bahari pana na kila mtu anaogelea kwa kadri awezavyo kupiga mbizi. Tujifunze tusiridhike na elimu ndogo ya mahusiano tuliyonayo. Tujitahidi kuyajua mahusiano kwa mapana yake. 👩‍❤️‍👩. 👫. 💃🏃🏻 Mungu atuwezeshe kujua yale tusiyoyajua. Mimi sio mtaalamu sana niache uwanja wazi wengine watasema zaidi.

Monday, May 30, 2016

MATAPELI WA FACEBOOK

Kuna wimbi kubwa la matapeli wa mitandaoni. Wengi wao hutumia majina feki,picha feki na baadhi ya vitu vya jinsi hiyo. Facebook imekuwa kinara wa tatizo hili pia. Nimependa makala hii ( bonyeza hapa ) itakusaidia pia.